balloon clan music bcm mfalme (feat. inkman bc) şarkı sözleri

Ayeee iNkmaN Heri nusu shari kuliko shari kamili Masalkheri, aheri Utamu wa mziki, bendi Maskini ni maskini tuu, hata katiba wakiamendi Mwanzo, kujiunga kidato ilikua balaa Si hela, si alama Nashuku irizi na ganga ganga za hao niitao familia, shuksha Lakini bado shukran, niliweza kujipigania Saa hii niko kwenye usukan Maisha hukuwa ni subra Msikize sultan, labda atakueleza kusiko dhiki abadaan kataan Ayee Ushairi ni utanashati wa muundo wala si mwandiko Bighairi ya bangi, me huvuta pumzi tuu Ushuzi si harufi bali hewa tuu Utunzi ndio baraka Mbaraka ni mtunzi Maneno sadaka tuu Mahindi na mtama zote nafaka tuu, lakini tui yenye fanaka ndio maziwa na vice versa Mchuzi tutaunywa iwe ni dagaa au papa, tofauti idadi ya vitunguu labda Moshi si moshi ka si ya shada Pochi la biashara ni rizla ndani, bandana, Balloon Clan family, purple ndo colour Flavour ni mbichwa tuu, favours doo Love hearts niko cardi boo iNkmaN daktari Marrapper ni sugu kama ugonjwa hatari lakini darasani wataketi, madaftari wataseti Hati ni moja tuu, wino na harufu ya damu Hao Corona mafua, me bado virusi vya ukedi utadedi mwanangu Na si siri, Mchele si staftahi, Ata kaburini msinifunge tai Ayee Chuo kikuu kilinifanya niwaone wahenga waongo Ati baada ya dhiki, faraja, sukuma baada ya sukuma, wiki imefika Ijumaa Upende usipende, chooni utachuchumaa... Utungo nlianza nikiwa tumboni sistuke mbona iNkmaN kakomaa Nadra sana kupata zabibu kwenye kapu la tufaha Malenga akinena, sogora na gonga gonga zake bado kwa kijiji ni mzaha Utamu wa pombe ni marafiki na furaha Twende bar basi Rhyme after rhyme, tamu ka na-na-si Tangu ukoloni ,kiberiti bado kifaru na fa-ra-si Mgema akisifiwa chunguza sticker labda unakunywa ma-ka-ma-si Bado swali nauliza, wapi mfalme? Nani mfalme? Simaanishi kutangaza vita lakini naangazia tuu, wapi mfalme? Zimepita miaka, zimebadilika karne, tumefika kenda, tulipita nane Tumezua zogo, mawe kwa afande Elfu noti ndio kipande Labda korti lakini utalala rumande Kwetu jangwani, tunaoga kwa umande Peace, nasimaanishi supu wala kamande. iNkmaN BC, the biggest Balloon.
Sanatçı: BALLOON CLAN MUSIC BCM
Türü: Belirtilmemiş
Ajans/Yapımcı: Belirtilmemiş
Şarkı Süresi: 3:26
Toplam: kayıtlı şarkı sözü
BALLOON CLAN MUSIC BCM hakkında bilgi girilmemiş.

Fotoğrafı