igambah sifa 2 şarkı sözleri
Mwambieni Mungu ni jinsi gani
Yalivyokutisha matendo yake
Uwezo wake ni mkuu kiasi kwamba
Adui wanyenyekea mbele zake
Mungu ametenda mema apewe sifa
Ahimidiwe, atukuzwe na achezewe
Imbeni utukufu wa jina lake
Mpeni sifa zake kwa utukufu
Shukrani zote zako Ee Ebenezer
Mahali nimefika ni nguvu zako
Nipanulie mipaka nifike mbali
Timiza ewe Bwana uliyoyasema
Mungu ametenda mema apewe sifa
Ahimidiwe, atukuzwe na achezewe
Imbeni utukufu wa jina lake
Mpeni sifa zake kwa utukufu
Nani alifanya hilo bahari kuwa nchi kavu?
Aah Aah Ni Mungu tu
Nani anayetawala kwa uwezo wake milele?
Aah Aah Ni Mungu tu
Nani macho yake huangalia mataifa yote?
Aah Aah Ni Mungu tu
Nani azuia miguu yetu isije teleza?
Aah Aah ni Mungu tu
Nani ameyahifadhi maisha yetu hadi sasa?
Aah Aah ni Mungu tu
Nani ajibiye maombi yetu yote kwa wakati ?
Aah Aah ni Mungu tu
Nani mfariji wetu wakati tuna machungu?
Aah Aah ni Mungu tu
Basi tuungane sote tumpe sifa zote kwani yeye
Aah Aah ni Mungu tu