nafsi huru trust nobody şarkı sözleri
Anza wewe kujiamini kabla hujawaamini wao
utashangaa, ukijiamini utakosa umuhimu wao
ni MaJudas na Delilah na zao ni makabaila
Focus yao ni hela utatumiwa kama tambara bovu
Ama toilet paper haja ikitimia wanasepa
unaemweka moyoni ndio mwenye uwezo wakuuvunja
chuja yupi mshkuja yupi wa kuja na mengine akulinde Jah
Roho za wengine wamemshinda Iddi Amin Dada
sio wema hao wandam kaa rada
Nashuku ibilisi ndio wanamfanyia ibada
Faya burn bad spirits ina waka shada
Kuna wale watakupa msaada dunia nzima wapakizee
na kuna wale ukipata faida inawauma watataka wakuumize
nasema trust nobody, Oya trust nobody sio wema wandam
TRust nobody ata kivuli chako hukukimbia ukiingia gizani
ata ulimi saingine hung'atwa wakati meno ni jirani
Akikufaa kwa dhiki adui je amekua rafiki mnafiki
hasidi hahitaji sababu vile gaidi hahitaji leseni kuharibu
utapata tabu usipojua mahesabu inabidi we
ufwate yako wakifwata yao
upange yako wakipanga yao
una njia zako wana njia zao
mbinu zao ndio mitego yao
jichunge nao ama upigwe bao
upigwe bao
Trust nobody sio wema wanadam
Wameshinda Wanyama kwa unyama
Trust Nobody

