ábella climate and heritage şarkı sözleri
Majanga ya asili yanamiminika
Ukame, joto na mafuriko kisha
Misitu inawaka, wanyama wanakwisha
tabia ya nchi kiukweli inatisha
Pwani unadhani hali vipi – tete
Mabadiliko ya tabia nchi yatutese
Udongo unakwenda, vijiji viswekwe
Yaani; Hali tete…Pwani pweke
makazi ya kando yanaharibika
Yanapigwa vimbunga na miamba kabisa
Mawimbi yakipiga, magofu yanalika
Ni nani mkunga wa kuwajibika
Na vipi zile ngome kongwe, mabaki na misikiti
Ebwana Eeeh! chondechonde tuione kizazi hiki
Na vile vizazi vijavyo wakawe wamiliki
Tuvitunze tukiwa tunavyo ili kesho wakavirithi
The climate is changing, Year to Year
And I see it’s changing decades to decades
I’m feeling hot, I’m feeling cold the climate is changing
The tides are high, eroding shore…The sea is rising
Majengo yaliyojengwa kwa matumbawe na chokaa
Ona yanavyosombwa na bahari maji yakijaa
Vyungu na sarafu mpaka shanga walizovaa
Tazama zinapotea pasipo hifadhi pata
Eeeeh.. Na Bado makazi tata, Maji yanatakataka
Na bado uvuvi tata,
bodaboda ndio biashara sasa
And now;
look at Karachi, Bombay to Manila
Cities are at risk Istanbul to Lima
In Rio de Janeiro the sea level rise
UK, SA..It affects world wide
Tushiriki kwa pamoja kutunza vilivyobaki
Tushapoteza viingi, na muda si rafiki safi
Tumehifadhi kwa maandishi, walau tuone picha basi
Kwa mfano natamani kuona miji ilivyotamaraki
Kama Bagamoyo, Songomnara, Zanzibar mpaka Sanje ya kati
Nipelekeni Mogadishu na Sofala au Kilwa Kisiwani kwenye bandari saaafi
Makutani I wapi? Nionesheni gati
Urithi wetu ndio hazina peke na pake yake iliyobaki
Tuulinde – urithi wetu
Tuutunze – Urithi wetu
Utulinde – Urithi Wetu
Ututunze – Maana ni wetu
The climate is changing, Year to Year
And I see it’s changing decades to decades
I’m feeling hot, I’m feeling cold the climate is changing
The tides are high, eroding shore…
The sea is rising
Tupande miti mikoko itusitiri,
makazi ya samaki dili
Tushapoteza vingi sio siri
Pamoja we can if we are willing
Teknolojia tuliyonayo tuitumie
Ile kidigitali Urithi wetu utunziwe
Vya kale mmh..! virekodiwe, Ili vizazi vyetu kesho visimuliwe
Climate change is a greatest risk facing us all
Join British Council initiatives,
Unite, Work together
Tackle climate change impacts
Transform our Worlds
Preserve our Pasts
Ensure one Future